John 12:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwa sababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo hazina.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yuda hakusema hivi kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi; ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha, na akawa akiiba zile fedha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Yuda hakusema hivyo kwa vile alikuwa anawajali sana maskini. Alisema hivyo kwa sababu alikuwa mwizi. Naye ndiye aliyetunza mfuko wa fedha za wafuasi wa Yesu. Naye mara kadhaa aliiba fedha kutoka katika mfuko huo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwa sababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo hazina.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwa sababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo hazina.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwivi, kwani ndiye aliyekuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwizi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwa sababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo hazina.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akisema hivyo, si kwa sababu ya kutunza maskini, ila kwa sababu ya kuwa mwizi; naye ndiye aliyeushika mfuko akivichukua, walivyopewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
(Hakusema maneno haya kwa sababu aliwasikilia wamasikini huruma, lakini kwa sababu alikuwa mwizi. Ni yeye aliyekuwa akichunga mufuko wa feza, naye alikuwa akijitwalia mali toka ndani yake.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Aliyasema haya, si kwa kuwahurumia maskini; hali kwa kuwa ni mwizi, nae ndiye aliyeshika mfuko, akavichikua vilivyotiwa humo.