John 13:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ilikuwa siku kabla ya sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua kwamba saa yake ya kuondoka ulimwenguni na kwenda kwa Baba ilikuwa imefika. Alikuwa amewapenda daima watu wake walioko duniani; naam, aliwapenda mpaka mwisho!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sikukuu ya Pasaka ilikuwa imekaribia. Isa alijua kuwa wakati wake wa kuondoka ulimwenguni ili kurudi kwa Baba umewadia. Alikuwa amewapenda watu wake waliokuwa ulimwenguni; naam, aliwapenda hadi mwisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sikukuu ya Pasaka ya Wayahudi ilikaribia. Yesu alijua kwamba wakati wake wa kuondoka ulimwenguni na kwenda kwa Baba ulikuwa umefika. Daima Yesu aliwapenda watu wa ulimwengu huu waliokuwa wake. Huu ulikuwa wakati alipowaonesha upendo wake mkuu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ilikuwa kabla ya sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua kwamba saa yake ya kuondoka ulimwenguni na kwenda kwa Baba ilikuwa imefika. Alikuwa amewapenda daima watu wake walioko duniani; naam, aliwapenda mpaka mwisho!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ilikuwa siku kabla ya sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua kwamba saa yake ya kuondoka ulimwenguni na kwenda kwa Baba ilikuwa imefika. Alikuwa amewapenda daima watu wake walioko duniani; naam, aliwapenda mpaka mwisho!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilikuwa mara tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua ya kuwa wakati wake wa kuondoka ulimwenguni ili kurudi kwa Baba umewadia. Alikuwa amewapenda watu wake waliokuwa ulimwenguni, naam, aliwapenda hadi kipimo cha mwisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilikuwa mara tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka. Isa alijua ya kuwa wakati wake wa kuondoka ulimwenguni ili kurudi kwa Baba umewadia. Alikuwa amewapenda watu wake waliokuwa ulimwenguni, naam, aliwapenda hadi kipimo cha mwisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, huku akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye akiwa amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ilikuwa siku kabla ya sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua kwamba saa yake ya kuondoka ulimwenguni na kwenda kwa Baba ilikuwa imefika. Alikuwa amewapenda daima watu wake walioko duniani; naam, aliwapenda mpaka mwisho!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Sikukuu ya Pasaka ilipokuwa haijatimia, Yesu alikuwa amejua, ya kuwa saa yake imefika, autoke ulimwengu huu, aende kwa Baba; kwa kuwa aliwapenda watu wake waliomo ulimwenguni, akawapenda mpaka mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa kumebaki siku moja mbele ya kutimia kwa sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua kwamba saa yake ya kutoka katika dunia na kurudi kwa Baba yake imetimia. Yeye alikuwa akiwapenda watu wake waliokuwa katika dunia, na akaendelea kuwapenda mpaka mwisho.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
HATTA kabla ya siku kuu ya Pasaka, Yesu akijua ya kuwa saa yake imefika atakayotoka katika ulimwengu huu kwenda kwa Baba, akiwa aliwapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapeuda ukomo wa upendo.