John 13:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Haya nisemayo hayawahusu nyinyi nyote. Mimi nawajua wale niliowachagua. Lakini lazima yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: ‘Yule aliyeshiriki chakula changu amegeuka kunishambulia.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sisemi hivi kuhusu ninyi nyote. Ninawajua wale niliowachagua. Lakini ni kutimiza andiko lisemalo, ‘Yeye aliyekula chakula changu ameinua kisigino chake dhidi yangu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nami sizungumzii habari zenu nyote. Nawafahamu watu wale niliowachagua. Lakini Maandiko yanapaswa kutimia kama yanavyosema: ‘Mtu aliyekula chakula pamoja nami amenigeuka.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Haya nisemayo hayawahusu ninyi nyote. Mimi nawajua wale niliowachagua. Lakini lazima yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: Yule aliyeshiriki chakula changu amegeuka kunishambulia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Haya nisemayo hayawahusu nyinyi nyote. Mimi nawajua wale niliowachagua. Lakini lazima yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: ‘Yule aliyeshiriki chakula changu amegeuka kunishambulia.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sisemi kuhusu ninyi nyote. Ninawajua wale niliowachagua. Lakini ni ili maandiko yapate kutimia, ‘Yeye aliyekula chakula changu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sisemi hivi kuhusu ninyi nyote. Ninawajua wale niliowachagua. Lakini ni ili Andiko lipate kutimia, kwamba, ‘Yeye aliyekula chakula changu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Haya nisemayo hayawahusu nyinyi nyote. Mimi nawajua wale niliowachagua. Lakini lazima yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: ‘Yule aliyeshiriki chakula changu amegeuka kunishambulia.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siyasemi ya ninyi nyote; mimi nawajua, niliowachagua. Lakini sharti andiko litimizwe la kwamba: Anayeula mkate wangu hunipiga mateke.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Sisemi juu ya ninyi wote; ninawajua wale niliowachagua. Lakini inafaa maneno haya yanayosemwa na Maandiko Matakatifu yatimie: ‘Yule aliyechangia chakula nami, amenigeuka.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sisemi khabari za ninyi nyote: nawajua niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aulae mkate pamoja nami ameinua kisigino chake juu yangu.