John 13:29 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kuwa Yuda alikuwa mweka hazina, baadhi yao walidhani kwamba Yesu alikuwa amemwambia anunue vilivyohitajiwa kwa sikukuu, au kwamba alikuwa amemwambia akatoe chochote kwa maskini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa Yuda alikuwa mtunza fedha, wengine walifikiri Isa alikuwa anamwambia akanunue vitu vilivyohitajika kwa ajili ya Sikukuu, au kuwapa maskini kitu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini kitu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa vile Yuda ndiye aliyekuwa msimamizi wa fedha zao, baadhi yao walidhani kuwa Yesu alikuwa na maana kuwa Yuda aende kununua vitu ambavyo wangehitaji kwa ajili ya sherehe. Au walidhani kuwa Yesu alitaka Yuda aende na kuwapa maskini cho chote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa kuwa Yuda alikuwa na wajibu wa kuutunza mfuko wa fedha, baadhi yao walidhani kwamba Yesu alikuwa amemwambia anunue vilivyohitajiwa kwa sikukuu, au kwamba alikuwa amemwambia akatoe chochote kwa maskini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kuwa Yuda alikuwa mweka hazina, baadhi yao walidhani kwamba Yesu alikuwa amemwambia anunue vilivyohitajiwa kwa sikukuu, au kwamba alikuwa amemwambia akatoe chochote kwa maskini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa Yuda alikuwa mtunza fedha, wengine walifikiri Yesu alikuwa amemwambia akanunue vitu vilivyohitajika kwa ajili ya Sikukuu, au kuwapa maskini cho chote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa Yuda alikuwa mtunza fedha, wengine walifikiri Isa alikuwa amemwambia akanunue vitu vilivyohitajika kwa ajili ya Sikukuu, au kuwapa maskini chochote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini kitu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kuwa Yuda alikuwa mweka hazina, baadhi yao walidhani kwamba Yesu alikuwa amemwambia anunue vilivyohitajiwa kwa sikukuu, au kwamba alikuwa amemwambia akatoe chochote kwa maskini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wengine wakawaza: kwa sababu Yuda aliushika mfuko wa senti, Yesu alimwambia: Nunua chakula cha siku za sikukuu! au agawie maskini kidogo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini kitu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wamoja walizani kama Yesu amemwambia aende kununua vitu walivyohitaji kwa sikukuu, au aende kuwasaidia wamasikini, kwa sababu Yuda ndiye aliyekuwa akichunga mufuko wa feza.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana wengine, kwa kuwa Yuda aliuchukua mfuko, walidhani ya kuwa Yesu alimwambia, Nunua tunavyovihitaji kwa siku kuu; au kwamba awape maskini kitu.