John 13:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watoto wangu, bado niko nanyi kwa muda mfupi tu. Mtanitafuta, lakini sasa nawaambieni yale niliyowaambia viongozi wa Wayahudi: ‘Niendako nyinyi hamwezi kwenda!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Watoto wangu, mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo. Mtanitafuta, na kama vile nilivyowaambia Wayahudi, vivyo hivyo sasa nawaambia na ninyi: Niendako, ninyi hamwezi kuja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akasema, “Watoto wangu, nitakuwa nanyi kwa kipindi kifupi tu kijacho. Nanyi mtanitafuta, lakini nawaambia sasa yale niliyowaambia viongozi wa Wayahudi: Kule niendako ninyi hamwezi kuja.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Watoto wangu, bado niko nanyi kwa muda mfupi tu. Mtanitafuta, lakini sasa nawaambieni yale niliyowaambia viongozi wa Wayahudi: Niendako ninyi hamwezi kwenda!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watoto wangu, bado niko nanyi kwa muda mfupi tu. Mtanitafuta, lakini sasa nawaambieni yale niliyowaambia viongozi wa Wayahudi: ‘Niendako nyinyi hamwezi kwenda!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Watoto wangu, mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo. Mtanitafuta na kama vile nilivyowaambia Wayahudi, vivyo hivyo sasa nawaambia na ninyi. Niendako, ninyi hamwezi kuja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Watoto wangu, mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo. Mtanitafuta, na kama vile nilivyowaambia Wayahudi, vivyo hivyo sasa nawaambia na ninyi. Niendako, ninyi hamwezi kuja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watoto wangu, bado niko nanyi kwa muda mfupi tu. Mtanitafuta, lakini sasa nawaambieni yale niliyowaambia viongozi wa Wayahudi: ‘Niendako nyinyi hamwezi kwenda!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vitoto, nipo pamoja nanyi bado kidogo; kisha mtanitafuta, lakini kama nilivyowaambia Wayuda: Ninyi hamwezi kupafika pale, ninapokwenda mimi, ndivyo, ninavyowaambia hata ninyi sasa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watoto wangu, ningali pamoja nanyi kwa muda mufupi tu. Mutanitafuta, lakini sawasawa nilivyowaambia Wayuda, ninawaambia ninyi vilevile kwamba hamuwezi kufika pahali ninapokwenda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Enyi watoto wachanga, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta: na kama nilivyowaambia Wayahudi, ya kama, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja: sasa nawaambia na ninyi.