John 13:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro akamwambia, “Wewe hutaniosha miguu kamwe!” Yesu akamjibu, “Nisipokuosha hutakuwa na uhusiano nami tena.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Petro akamwambia, “La, wewe hutaninawisha miguu kamwe.” Isa akamjibu, “Kama nisipokunawisha, wewe huna sehemu nami.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro akasema, “Hapana! Huwezi kamwe kuniosha miguu yangu kamwe.” Yesu akamjibu, “Kama sitakuosha miguu yako, basi hutakuwa miongoni mwa watu wangu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro akamwambia, “Wewe hutaniosha miguu kamwe!” Yesu akamjibu, “Nisipokuosha hutakuwa na uhusiano nami tena.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro akamwambia, “Wewe hutaniosha miguu kamwe!” Yesu akamjibu, “Nisipokuosha hutakuwa na uhusiano nami tena.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Petro akamwambia, “La, wewe hutaninawisha miguu kamwe.” Yesu akamjibu, “Kama nisipokunawisha, wewe huna sehemu nami.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Petro akamwambia, “La, wewe hutaninawisha miguu kamwe.” Isa akamjibu, “Kama nisipokunawisha, wewe huna sehemu nami.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Petro akamwambia, Wewe hutaniosha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Nisipokuosha, huna shirika nami.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro akamwambia, “Wewe hutaniosha miguu kamwe!” Yesu akamjibu, “Nisipokuosha hutakuwa na uhusiano nami tena.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Petero alipomwambia: Hutaniosha miguu kale na kale, Yesu akamjibu: Nisipokuosha, hakuna fungu lako tena lililoko kwangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Petro akamwambia: “Hautanawisha miguu yangu hata kidogo!” Yesu akamujibu: “Nisipokunawisha miguu, hauna ushirika pamoja nami.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Petro akamwambia. Hutanitawadha miguu milele. Yesu akamwambia, Nisipokutawadha, huna fungu pamoja nami.