John 14:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu yeyote asiyenipenda hayashiki maneno yangu, na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini yeyote asiyenipenda hafuati mafundisho yangu. Mafundisho haya mnayosikia kwa hakika siyo yangu. Ni kutoka kwa Baba yangu aliyenituma.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu ye yote asiyenipenda hayashiki maneno yangu na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu yeyote asiyenipenda hayashiki maneno yangu na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenituma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asiyenipenda hayashiki maneno yangu; nalo Neno, mnalolisikia, silo langu, ila la Baba aliyenituma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno munalosikia nikisema halitoki kwangu, lakini linatoka kwa Baba yangu aliyenituma.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Asiyenipenda, hayashiki maneno yangu; na neno mnalolisikia silo langu, bali lake Baba aliyenipeleka.