John 14:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mlikwisha sikia nikiwaambieni: ‘Ninakwenda zangu, kisha nitarudi tena kwenu.’ Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwa Baba, maana yeye ni mkuu kuliko mimi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mlisikia nikisema, ‘Ninaenda zangu, lakini nitarudi tena.’ Kama kweli mngenipenda, mngefurahi kwa kuwa naenda kwa Baba, kwani Baba ni mkuu kuliko mimi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mlinisikia nikiwaambia, ‘Naondoka, lakini nitakuja tena kwenu.’ Mngenipenda, mngefurahi kuwa naenda kwa Baba, kwa sababu Baba ni mkuu kuliko mimi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mlikwisha sikia nikiwaambieni: Ninakwenda zangu, kisha nitarudi tena kwenu. Kama mngalinipenda mngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwa Baba, maana yeye ni mkuu kuliko mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mlikwisha sikia nikiwaambieni: ‘Ninakwenda zangu, kisha nitarudi tena kwenu.’ Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwa Baba, maana yeye ni mkuu kuliko mimi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mlinisikia nikisema, ‘Ninakwenda zangu, lakini nitarudi tena.’ Kama kweli mngelinipenda mngelifurahi kwa kuwa nakwenda kwa Baba, kwani Baba ni mkuu kuliko mimi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mlinisikia nikisema, ‘Ninakwenda zangu, lakini nitarudi tena.’ Kama kweli mngelinipenda mngelifurahi kwa kuwa naenda kwa Baba, kwani Baba ni mkuu kuniliko mimi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mlisikia ya kwamba mimi niliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mlikwisha sikia nikiwaambieni: ‘Ninakwenda zangu, kisha nitarudi tena kwenu.’ Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwa Baba, maana yeye ni mkuu kuliko mimi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmesikia, nilivyowaambia: Nakwenda zangu, tena nitawajia. Kama mngenipenda, mngefurahi, ya kuwa nakwenda kwa Baba, kwani Baba ni mkubwa kuliko mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumesikia jinsi nilivyowaambia kwamba ninajiendea, lakini nitawarudilia tena. Kama mungenipenda, mungefurahia kujua kwamba ninakwenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mukubwa kuliko mimi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Nakwenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi, kwa sababu nashika njia kwenda kwa Baba: kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.