John 15:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi hamkunichagua mimi; mimi niliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda, matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapeni chochote mnachomwomba kwa jina langu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu. Ili nalo lolote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninyi hamkunichagua mimi. Bali ni mimi niliyewachagua ninyi. Nami niliwapa kazi hii: Kwenda na kutoa matunda; matunda ambayo yatadumu. Ndipo Baba atakapowapa chochote mtakachomwomba katika jina langu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi hamkunichagua mimi; mimi niliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda, matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapa ninyi chochote mumwombacho kwa jina langu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi hamkunichagua mimi; mimi niliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda, matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapeni chochote mnachomwomba kwa jina langu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu. Ili nalo lolote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape ninyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lolote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi hamkunichagua mimi; mimi niliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda, matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapeni chochote mnachomwomba kwa jina langu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sio ninyi mlionichagua, lakini ndiye mimi niliyewachagua ninyi, nikawaweka, mwende kuzaa matunda, nayo matunda yenu yakae; kwa hiyo Baba atawapa lo lote, mtakalomwomba katika Jina langu.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi hamukunichagua mimi, lakini ni mimi niliyewachagua ninyi. Nami nimewatuma muende kuzaa matunda yasiyokuwa na mwisho. Kwa hiyo Baba atawapa chochote munachoomba kwa jina langu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi, nikawaamuru, mwende zenu mkazae, mazao yenu yakakae: illi lo lote mmwombalo Baba kwa Jina langu, awapeni.