John 15:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda yeye huliondoa, na kila tawi lizaalo hulisafisha lipate kuzaa zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata, nalo kila tawi linalozaa, hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yeye hulikata kutoka kwangu kila tawi lisilozaa matunda. Pia hupunguza majani katika kila tawi linalozaa matunda ili kuliandaa liweze kuzaa matunda zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye huliondoa ndani yangu kila tawi lisilozaa matunda, na kila tawi lizaalo hulisafisha lipate kuzaa zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda yeye huliondoa, na kila tawi lizaalo hulisafisha lipate kuzaa zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata, nalo kila tawi lizaalo, hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata, nalo kila tawi lizaalo, hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda yeye huliondoa, na kila tawi lizaalo hulisafisha lipate kuzaa zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila tawi langu lisilozaa huliondoa; lakini kila tawi lizaalo hulitakasa akilipogoa, lipate kuzaa mengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye anakata kila tawi linalokuwa ndani yangu lisilozaa matunda. Naye anasafisha kila tawi linalozaa matunda, kusudi lizae matunda mengi zaidi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kilia tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na killa lizaalo hulisafisha illi lizidi kuzaa.