John 15:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama nisingalikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia; lakini sasa hawawezi kujitetea kwamba hawana dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama sikuja na kusema nao, hawangekuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa hawana udhuru kwa ajili ya dhambi zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kama nisingekuwa nimekuja na kusema na watu wa ulimwengu, basi wasingekuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa nimekwisha sema nao. Hivyo hawana cha kisingizio cha dhambi zao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama nisingalikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia; lakini sasa hawawezi kujitetea kwamba hawana dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama nisingalikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia; lakini sasa hawawezi kujitetea kwamba hawana dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama sikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa hawana udhuru kwa ajili ya dhambi zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama sikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa hawana udhuru kwa ajili ya dhambi zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana kisingizio kwa dhambi yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama nisingalikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia; lakini sasa hawawezi kujitetea kwamba hawana dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama singalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na kosa; lakini sasa hawana, watakalojikania makosa yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama singekuja kusema nao, wasingekuwa na zambi; lakini sasa hawataweza kukana zambi yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kama singalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; sasa hawana udhuru kwa dhamhi yao.