John 15:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Baba yangu hutukuzwa kwa vile mnavyozaa matunda mengi, nanyi mtajidhihirisha kuwa wanafunzi wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninyi mdhihirishe kuwa mmekuwa wafuasi wangu kwa kutoa matunda mengi. Kwani hiyo itamletea Baba utukufu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Baba yangu hutukuzwa, kwa vile mzaavyo matunda mengi, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Baba yangu hutukuzwa, kwa vile mzaavyo matunda mengi, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo ndipo, Baba yangu anapotukuzwa, mnapozaa mengi, mkawa wanafunzi wangu.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mukizaa matunda mengi, Baba yangu atatukuzwa, na hivi mutakuwa kweli wanafunzi wangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa hiyo atukuzwa Baba yangu, mzae sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.