John 16:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo baadhi ya wanafunzi wake wakaulizana, “Ana maana gani anapotuambia: ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?’ Tena anasema: ‘Kwa kuwa ninakwenda kwa Baba!’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona’? Naye ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninaenda kwa Baba’?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi baadhi ya wanafunzi wake wakasemezana, Neno gani hilo asemalo, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? Na hilo, Kwa sababu naenda zangu kwa Baba?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya wafuasi wake wakaambiana wao kwa wao, “Ana maana gani anaposema, ‘Baada ya kipindi kifupi hamtaniona tena. Kisha baada ya kipindi kifupi kingine mtaniona tena?’ Tena ana maana gani anaposema, ‘Kwa sababu naenda kwa Baba’?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo baadhi ya wanafunzi wake wakaulizana, “Ana maana gani anapotwambia: Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona? Tena anasema: Kwa kuwa ninakwenda kwa Baba!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo baadhi ya wanafunzi wake wakaulizana, “Ana maana gani anapotuambia: ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?’ Tena anasema: ‘Kwa kuwa ninakwenda kwa Baba!’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona?’ Naye ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa Baba?’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona?’ Naye ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa Baba?’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi baadhi ya wanafunzi wake wakasemezana, Neno gani hilo asemalo, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? Na hilo, Kwa sababu naenda zangu kwa Baba?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo baadhi ya wanafunzi wake wakaulizana, “Ana maana gani anapotuambia: ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?’ Tena anasema: ‘Kwa kuwa ninakwenda kwa Baba!’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, kulikuwako wanafunzi wake waliosemezana wao kwa wao: Neno hili, analotuambia, ni neno gani la kwamba: Bado kidogo hamtaniona, tena patakapopita kidogo, mtaniona? Na tena: Ninakwenda kwa Baba?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi baadhi ya wanafunzi wake wakasemezana, Neno gani hilo asemalo, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? Na hilo, Kwa sababu naenda zangu kwa Baba?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wanafunzi wake wamoja wakasemezana hivi: “Yeye anatuambia kwamba kunabakia wakati kidogo nasi hatutamwona, lakini kisha wakati kidogo tutamwona tena. Vilevile anasema kwamba ni kwa sababu anakwenda kwa Baba yake. Maana ya maneno haya yote ni nini?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi baadhi ya wanafunzi wake walisemezana, Neno gani hili analosema, Bado kitambo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo na mtaniona? na, Kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba?