John 16:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi pia mna huzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyi mtajaa furaha mioyoni mwenu, na furaha hiyo hakuna mtu atakayeiondoa kwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndivyo ilivyo hata kwenu pia. Sasa mna huzuni lakini nitawaona tena, nanyi mtafurahi. Mtakuwa na furaha ambayo hakuna mtu atakayewaondolea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi pia mna huzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyi mtajaa furaha mioyoni mwenu, na furaha hiyo hakuna mtu atakayeiondoa kwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi pia mna huzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyi mtajaa furaha mioyoni mwenu, na furaha hiyo hakuna mtu atakayeiondoa kwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi na furaha yenu hakuna awaondoleaye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi na furaha yenu hakuna awaondoleaye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi pia mna huzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyi mtajaa furaha mioyoni mwenu, na furaha hiyo hakuna mtu atakayeiondoa kwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, nanyi sasa mnasikitika, lakini tutaonana tena, ndipo, mioyo yenu itakapofurahi; hiyo furaha yenu hakuna atakayeiondoa kwenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na sasa ninyi vilevile munasikia uchungu, lakini nitawaona tena, nanyi mutafurahi, wala hakuna mutu atakayeweza kuwahuzunisha tena.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi na ninyi sasa hivi mna huzuni; lakini nitawaona tena, na moyo wenu utafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleae.