John 16:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo hamtaniomba chochote. Kweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu, atawapeni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin nawaambia, mkimwomba Baba jambo lolote kwa jina langu, yeye atawapa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika siku hiyo, hamtapaswa kuniuliza mimi kitu chochote. Nami kwa hakika nawaambia, Baba yangu atawapa lo lote mtakalomwomba kwa jina langu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku hiyo hamtaniomba chochote. Kweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu, atawapeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo hamtaniomba chochote. Kweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu, atawapeni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin nawaambia, kama mkimwomba Baba jambo lo lote kwa Jina langu, yeye atawapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin nawaambia, kama mkimwomba Baba jambo lolote kwa jina langu, yeye atawapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa jina langu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo hamtaniomba chochote. Kweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu, atawapeni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ile hamtaniuliza neno.* *Kweli kweli nawaambiani: Lo lote, mtakalomwomba Baba, atawapa katika Jina langu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Siku ile itakapotimia, ninyi hamutaniuliza juu ya kitu fulani. Kweli, kweli ninawaambia: Baba atawapa chochote mutakachomwomba kwa jina langu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na siku ile hamtaniuliza neno. Amin, amin, nawaambieni, Mkimwomba Baba neno kwa jina langu atawapeni.