John 16:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hadi sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hamjawahi kuomba lo lote kwa namna hii hapo awali. Bali ombeni kwa jina langu nanyi mtapewa. Kisha mtakuwa na furaha iliyotimia ndani yenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mpaka sasa hamjaomba jambo lo lote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mpaka sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mpaka leo hakuna, mliloliomba katika Jina langu. Ombeni! Ndipo, mtakapopewa, furaha yenu iwe imetimizwa yote!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mpaka sasa hamujaomba kitu kwa jina langu. Muombe, nanyi mutapewa, na furaha yenu itakuwa kubwa kabisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mpaka leo hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, na mtapata, furaha yenu iwe timilifu.