John 16:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo nyinyi nyote mtatawanywa kila mtu kwake, nami nitaachwa peke yangu. Kumbe, lakini mimi siko peke yangu, maana Baba yu pamoja nami.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Saa inakuja, naam, imekwisha kuwadia, mtakapotawanyika kila mmoja kwenda nyumbani mwake na kuniacha peke yangu. Lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yu pamoja nami.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Basi nisikilizeni! Wakati unakuja mtakapotawanywa, kila mmoja nyumbani kwake. Kwa hakika, wakati huo tayari umekwisha fika. Ninyi mtaniacha, nami nitabaki peke yangu. Lakini kamwe mimi siko peke yangu, kwa sababu Baba yupo pamoja nami.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo ninyi nyote mtatawanyika kila mtu kwake, nami nitaachwa peke yangu. Kumbe, lakini mimi siko peke yangu, maana Baba yu pamoja nami.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo nyinyi nyote mtatawanywa kila mtu kwake, nami nitaachwa peke yangu. Kumbe, lakini mimi siko peke yangu, maana Baba yu pamoja nami.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Saa inakuja, naam, imekwisha kuwadia, mtakapotawanyika kila mmoja kwenda nyumbani kwake na kuniacha peke yangu. Lakini mimi si peke yangu kwa sababu Baba yu pamoja nami.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Saa inakuja, naam, imekwisha kuwadia, mtakapotawanyika kila mmoja kwenda nyumbani kwake na kuniacha peke yangu. Lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yu pamoja nami.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, saa inakuja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; lakini mimi siko peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo nyinyi nyote mtatawanywa kila mtu kwake, nami nitaachwa peke yangu. Kumbe, lakini mimi siko peke yangu, maana Baba yu pamoja nami.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazameni, saa inakuja, tena imekwisha fika, mtawanyike kila mtu na kwao kwenyewe, mniache mimi, niwe peke yangu. Lakini mimi sipo peke yangu, kwani Baba yupo pamoja nami.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutakuwa wakati, nao umetimia, ndio wakati mutakaposambazwa, kila mutu akijiendea ngambo yake mwenyewe, nanyi mutaniacha peke yangu. Lakini mimi si peke yangu kabisa, kwa sababu Baba yuko pamoja nami.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Saa inakuja, naam, imekwisha kuja, mtatawanyika killa mmoja kwa mambo yake, mtaniacha mimi peke yangu; wala mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.