John 17:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa nakuja kwako. Mimi sitakaa ulimwenguni, lakini hawa wafuasi wangu bado wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu, uwaweke hao salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Ndipo watapokuwa na umoja, kama vile mimi na wewe tulivyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni, kwani mimi nakuja kwako. Baba Mtakatifu, walinde, wakae na Jina lako, ulilonipa, wapate kuwa mmoja wote, kama sisi tulivyo mmoja!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi sitabaki tena katika dunia, lakini wao wangali katika dunia na mimi ninakuja kwako. Baba Mutakatifu, uwalinde kwa uwezo wa jina lako, lile jina ulilonipa, kusudi wakuwe mumoja kama vile sisi tunavyokuwa mumoja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mimi simo tena ulimwenguni, na hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, uwalinde kwa jina lako wale ulionipa; wawe moja, kama sisi.