John 17:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule mwana mpotevu, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa upotevu, ili Maandiko yapate kutimia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilipokuwa pamoja nao niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Niliwalinda. Ni mmoja wao tu aliyepotea; yule ambaye kwa hakika angelikuja kupotea. Hii ilikuwa hivyo ili kuonesha ukweli wa yale yaliyosemwa na Maandiko kuwa yangetokea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule aliyelazimika kupotea ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule mwana mpotevu, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa, ili Maandiko yapate kutimia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa upotevu, ili Maandiko yapate kutimia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilipokuwapo pamoja nao, mimi niliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule mwana mpotevu, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipokuwa pamoja nao naliwalinda, wakae na Jina lako, ulilonipa, nikawaangalia. Nao hawakuangamia hata mmoja wao, pasipo yule mwana wa mwangamizo, yaliyoandikwa yapate kutimia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda kwa uwezo wa jina lako, ndilo lile jina ulilonipa. Nimewachunga wala hakuna mumoja wao aliyepotea, isipokuwa yule anayepaswa kupotea, kusudi Maandiko Matakatifu yatimizwe.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nilipokuwa pamoja nao ulimwenguni, mimi naliwalinda kwa jina lako: wale ulionipa naliwatunza, wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, illa yule mwana wa upotevu maandiko yapate kutimizwa.