John 17:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako. Wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiwe uliyenituma mimi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baba, naomba kwamba wote wanaoniamini waungane pamoja na kuwa na umoja. Wawe na umoja kama vile wewe na mimi tulivyoungana; wewe umo ndani yangu nami nimo ndani yako. Nami naomba nao pia waungane na kuwa na umoja ndani yetu. Ndipo ulimwengu nao utaamini kuwa ndiwe uliyenituma.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako, wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiye uliyenituma mimi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako, wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiwe uliyenituma mimi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wote wapate kuwa mmoja, kama ulivyomo mwangu, wewe Baba, nami nilivyomo mwako! Wapate kuwamo mwetu nao hao, ulimwengu upate kunitegemea, ya kuwa wewe umenituma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninaomba kusudi wote wakuwe mumoja, kama vile wewe Baba unavyokuwa ndani yangu na mimi ndani yako. Ninaomba vilevile kwamba wakuwe ndani yetu, kusudi dunia ipate kuamini kwamba umenituma.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wote wawe umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako, illi na hawa wawe umoja ndani yetu: ulimwengu upate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.