John 17:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu; naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda wao kama unavyonipenda mimi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi ndani yao na wewe ndani yangu: ili wawe wamekamilika katika umoja, na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda mimi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nitakuwa ndani yao, nawe utakuwa ndani yangu. Hivyo watakuwa na umoja kamili. Kisha ulimwengu utajua kwamba wewe ndiwe uliyenituma na ya kuwa uliwapenda jinsi ulivyonipenda mimi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu; naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda wao kama unavyonipenda mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu; naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda wao kama unavyonipenda mimi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi ndani yako na wewe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda mimi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi ndani yako na wewe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda mimi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu; naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda wao kama unavyonipenda mimi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi niwemo mwao, nawe wewe uwemo mwangu, wawe watu waliomaliza kuwa mmoja, nao ulimwengu utambue, ya kuwa wewe umenituma, kisha umewapenda, kama ulivyonipenda mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninaomba nikuwe ndani yao na wewe ndani yangu, kusudi wapate kuwa mumoja kabisa; na dunia ijue kama wewe ndiwe uliyenituma na kwamba unawapenda kama vile unavyonipenda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, wapate kukamilika na kuwa umoja; illi ulimwengu ujue ya kuwa udiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.