John 17:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na uhai wa milele ndio huu: Kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe uliye Mungu wa pekee wa kweli, na Isa Al-Masihi uliyemtuma.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na uzima wa milele ndiyo huu: kwamba watu watakujua wewe, Mungu pekee wa kweli, na kwamba watamjua Yesu Kristo, Yeye uliyemtuma.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na uzima wa milele ndio huu: kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na uhai wa milele ndio huu: kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mwenyezi Mungu wa pekee wa kweli, na Isa Al-Masihi uliyemtuma.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na uhai wa milele ndio huu: Kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao huu ndio uzima wa kale na kale, wakutambue wewe, kwamba ndiwe peke yako Mungu wa kweli, tena wamtambue yule, uliyemtuma, kwamba ndiye Yesu Kristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao uzima wa milele ni kukujua wewe unayekuwa peke yako Mungu wa kweli na Yesu Kristo uliyemutuma.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.