John 18:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Simoni Petro alikuwa na upanga; basi, akauchomoa, akamkata sikio la kulia mtumishi wa kuhani mkuu. Mtumishi huyo aliitwa Malko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Simoni Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kuume mtumishi wa kuhani mkuu. (Mtumishi huyo aliitwa Malko.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. Na yule mtumwa jina lake ni Malko.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Simoni Petro akauchomoa upanga aliokuwa ameufunga kiunoni. Akampiga nao mtumishi wa Kuhani Mkuu, na kulikata sikio lake la kulia. (Jina la mtumishi huyo lilikuwa ni Maliko.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Simoni Petro alikuwa na upanga; basi, akauchomoa, akamkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani Mkuu. Mtumishi huyo aliitwa Malko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Simoni Petro alikuwa na upanga; basi, akauchomoa, akamkata sikio la kulia mtumishi wa kuhani mkuu. Mtumishi huyo aliitwa Malko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Simoni Petro aliyekuwa na upanga akaufuta na kumkata sikio la kuume mtumishi wa Kuhani Mkuu. Jina la mtumishi huyo aliitwa Malko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Simoni Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kuume mtumishi wa kuhani mkuu. Jina la mtumishi huyo aliitwa Malko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kulia. Na yule mtumwa jina lake ni Malko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Simoni Petro alikuwa na upanga; basi, akauchomoa, akamkata sikio la kulia mtumishi wa kuhani mkuu. Mtumishi huyo aliitwa Malko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Simoni Petero alikuwa na upanga, akauchomoa, akampiga mtumwa wa mtambikaji mkuu, akamkata sikio la kuume; jina lake yule mtumwa ndiye Malko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. Na yule mtumwa jina lake ni Malko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Simoni Petro alikuwa na upanga, akauchomoa na kumukata mutumishi wa Kuhani Mukubwa sikio la kuume. (Jina la mutumishi yule lilikuwa Malko.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Simon Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumishi wa kuhani mkuu akamkata sikio lake la kuume. Na yule mtumishi jina lake alikwitwa Malko.