John 18:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyo mwanafunzi mwingine alikuwa anajulikana kwa kuhani mkuu, hivyo aliingia pamoja na Yesu ndani ya ukumbi wa kuhani mkuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walikuwa wakimfuata Isa. Huyu mwanafunzi mwingine alikuwa anafahamika kwa kuhani mkuu, hivyo aliingia uani kwa kuhani mkuu pamoja na Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamfuata Yesu, Petro na mwanafunzi mwingine. Na mwanafunzi huyo alikuwa amejulikana na Kuhani Mkuu, akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani Mkuu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Simoni Petro na mmoja wa wafuasi wengine wa Yesu walienda pamoja na Yesu. Mfuasi huyu alimfahamu kuhani mkuu. Hivyo akaingia pamoja na Yesu ndani ya uwanja wa nyumba ya kuhani mkuu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyo mwanafunzi mwingine alikuwa anajulikana kwa Kuhani Mkuu, hivyo aliingia pamoja na Yesu ndani ya ukumbi wa Kuhani Mkuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyo mwanafunzi mwingine alikuwa anajulikana kwa kuhani mkuu, hivyo aliingia pamoja na Yesu ndani ya ukumbi wa kuhani mkuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walikuwa wakimfuata Yesu. Huyu mwanafunzi mwingine alikuwa anafahamika kwa Kuhani Mkuu, hivyo aliingia ndani ya ukumbi pamoja na Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walikuwa wakimfuata Isa. Huyu mwanafunzi mwingine alikuwa anafahamika kwa kuhani mkuu, hivyo aliingia ndani ya ukumbi pamoja na Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamfuata Yesu, Petro na mwanafunzi mwingine. Na mwanafunzi huyo alikuwa amejulikana na Kuhani Mkuu, akaingia pamoja na Yesu katika ukumbi wa Kuhani Mkuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyo mwanafunzi mwingine alikuwa anajulikana kwa kuhani mkuu, hivyo aliingia pamoja na Yesu ndani ya ukumbi wa kuhani mkuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Simoni Petero na mwanafunzi mwingine wakamfuata Yesu; yule mwanafunzi mwingine alikuwa amejuana na mtambikaji mkuu, akaingia pamoja na Yesu uani kwa mtambikaji mkuu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamfuata Yesu, Petro na mwanafunzi mwingine. Na mwanafunzi huyo alikuwa amejulikana na Kuhani Mkuu, akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani Mkuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Simoni Petro na mwanafunzi mwingine walimufuata Yesu. Yule mwanafunzi alikuwa akijulikana na Kuhani Mukubwa, kwa hiyo akaingia pamoja na Yesu ndani ya upango wa nyumba ya Kuhani Mukubwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Simon Petro akamfuata Yesu, na mwanafunzi mwingine: na yule mwanafunzi alikuwa anajulika na kuhani mkuu: akaingia pamoja na Yesu behewani mwa kuhani mkuu; lakini Petro akasimama nje mlangoni.