John 18:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Petro alikuwa amesimama nje, karibu na mlango. Basi, huyo mwanafunzi mwingine aliyekuwa anajulikana kwa kuhani mkuu alitoka nje akasema na mjakazi, mngojamlango, akamwingiza Petro ndani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Petro alisimama nje karibu na lango. Ndipo yule mwanafunzi mwingine, aliyejulikana na kuhani mkuu, akazungumza na msichana aliyekuwa analinda lango, akamruhusu Petro aingie ndani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Petro akasimama nje mlangoni. Basi yule mwanafunzi mwingine aliyejulikana na Kuhani Mkuu akatoka, akasema na mngoja mlango, akamleta Petro ndani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Petro alisubiri nje karibu na mlango. Yule mfuasi aliyemjua kuhani mkuu alirudi nje na kuongea na mlinda mlango. Kisha alimleta Petro ndani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Petro alikuwa amesimama nje, karibu na mlango. Basi, huyo mwanafunzi mwingine aliyekuwa anajulikana kwa Kuhani Mkuu alitoka nje akasema na mjakazi, mngoja mlango, akamwingiza Petro ndani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Petro alikuwa amesimama nje, karibu na mlango. Basi, huyo mwanafunzi mwingine aliyekuwa anajulikana kwa kuhani mkuu alitoka nje akasema na mjakazi, mngojamlango, akamwingiza Petro ndani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Petro alisimama nje karibu na lango, ndipo yule mwanafunzi mwingine akazungumza na msichana aliyekuwa analinda lango, akamruhusu Petro aingie ndani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Petro alisimama nje karibu na lango, ndipo yule mwanafunzi mwingine, aliyejulikana na kuhani mkuu, akazungumza na msichana aliyekuwa analinda lango, akamruhusu Petro aingie ndani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Petro akasimama nje mlangoni. Basi yule mwanafunzi mwingine aliyejulikana na Kuhani Mkuu akatoka, akasema na mlinda mlango, akamleta Petro ndani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Petro alikuwa amesimama nje, karibu na mlango. Basi, huyo mwanafunzi mwingine aliyekuwa anajulikana kwa kuhani mkuu alitoka nje akasema na mjakazi, mngojamlango, akamwingiza Petro ndani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Petero akasimama nje mlangoni. Yule mwanafunzi mwingine aliyejuana na mtambikaji mkuu akatoka, akasema na mlinda mlango, akamwingiza Petero.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Petro akasimama nje mlangoni. Basi yule mwanafunzi mwingine aliyejulikana na Kuhani Mkuu akatoka, akasema na mngoja mlango, akamleta Petro ndani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Petro alisimama inje karibu na mulango. Yule mwanafunzi mwingine, aliyejulikana na Kuhani Mukubwa, akatoka inje, akasema na mwanamuke aliyelinda mulango, naye akamwachilia Petro kuingia ndani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi yule mwanafunzi mwingine aliyejulika na kuhani mkuu akatoka akasema na mwanamke aliye mngoje mlango, akamleta Petro ndani.