John 18:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo mjakazi mngojamlango akamwuliza Petro, “Je, nawe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro akamwambia, “Si mimi!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule msichana akamuuliza Petro, “Je, wewe pia si mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro akajibu, “Sio mimi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi yule kijakazi, aliyekuwa mngoja mlango, akamwambia Petro, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu? Naye akasema, Si mimi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Msichana aliyekuwepo langoni alimwambia Petro, “Je! Wewe pia ni mmoja wa wafuasi wa mtu yule?” Petro akajibu, “Hapana, mimi siye!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo msichana mngoja mlango akamwuliza Petro, “Je, nawe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro akamwambia, “Si mimi!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo mjakazi mngojamlango akamwuliza Petro, “Je, nawe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro akamwambia, “Si mimi!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule msichana akamwuliza Petro, “Je, wewe pia si mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro akajibu, “Mimi sio.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule msichana akamuuliza Petro, “Je, wewe pia si mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro akajibu, “Sio mimi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi yule kijakazi, aliyekuwa mlinda mlango, akamwambia Petro, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu? Naye akasema, Si mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo mjakazi mngojamlango akamwuliza Petro, “Je, nawe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro akamwambia, “Si mimi!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha kijakazi aliyekuwa mlinda mlango alipomwambia Petero: Wewe nawe humo miongoni mwao wanafunzi wa mtu huyo? akasema: Simo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi yule kijakazi, aliyekuwa mngoja mlango, akamwambia Petro, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu? Naye akasema, Si mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mwanamuke akamwambia Petro: “Wewe vilevile si mumoja wa wanafunzi wa mutu huyu?” Petro akamujibu: “Hapana! Mimi si mwanafunzi wake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi yule kijakazi aliye mngoje mlango akamwambia Petro, Wewe nawe, je! huwi mmojawapo wa wanafunzi wake mtu huyu? Yeye akasema, Si mimi.