John 18:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yuda, aliyemsaliti Yesu, alipajua mahali hapo kwani mara nyingi Yesu alikutana na wanafunzi wake huko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Yuda, aliyemsaliti, alipafahamu mahali hapo, kwani Isa alikuwa akikutana humo na wanafunzi wake mara kwa mara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yuda, yule aliyehusika kumsaliti Yesu, alipafahamu mahali pale. Alipajua kwa sababu Yesu mara nyingi alikutana na wafuasi wake pale.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yuda, aliyemsaliti Yesu, alipajua mahali hapo kwani mara nyingi Yesu alikutana na wanafunzi wake huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yuda, aliyemsaliti Yesu, alipajua mahali hapo kwani mara nyingi Yesu alikutana na wanafunzi wake huko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Yuda, yule aliyemsaliti alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana humo na wanafunzi wake mara kwa mara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Yuda, yule aliyemsaliti alipafahamu mahali hapo kwani Isa alikuwa akikutana humo na wanafunzi wake mara kwa mara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yuda, aliyemsaliti Yesu, alipajua mahali hapo kwani mara nyingi Yesu alikutana na wanafunzi wake huko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini naye Yuda aliyemchongea alipajua hapo, kwani Yesu na wanafunzi wake walikusanyika mara nyingi hapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yuda, yule aliyekuwa amemutoa, alijua pahali pale, kwa sababu Yesu alikuwa akikutana kule mara nyingi pamoja na wanafunzi wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yuda nae, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikwenda huko marra nyingi pamoja na wanafunzi wake.