John 18:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akamjibu, “Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundisha katika masunagogi na hekaluni, mahali wanapokutana Wayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamjibu, “Nimekuwa nikizungumza waziwazi mbele ya watu wote. Siku zote nimefundisha katika masinagogi na Hekaluni, mahali Wayahudi wote hukusanyika. Sikusema jambo lolote kwa siri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nalifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala kwa siri mimi sikusema neno lo lote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akamjibu, “Daima nimesema wazi kwa watu wote. Siku zote nimefundisha kwenye masinagogi na kwenye eneo la Hekalu. Wayahudi wote hukusanyika pale. Sijawahi kusema jambo lo lote kwa siri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akamjibu, “Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundisha katika masunagogi na Hekaluni, mahali wakutanikiapo Wayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akamjibu, “Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundisha katika masunagogi na hekaluni, mahali wanapokutana Wayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamjibu, “Nimekuwa nikizungumza waziwazi mbele ya watu wote. Siku zote nimefundisha katika masinagogi na Hekaluni mahali ambapo Wayahudi wote hukusanyika. Sikusema jambo lo lote kwa siri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamjibu, “Nimekuwa nikizungumza waziwazi mbele ya watu wote. Siku zote nimefundisha katika masinagogi na Hekaluni, mahali ambapo Wayahudi wote hukusanyika. Sikusema jambo lolote kwa siri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; siku zote nilifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala mimi sikusema neno lolote kwa siri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akamjibu, “Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundisha katika masunagogi na hekaluni, mahali wanapokutana Wayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akamjibu: Mimi nimesema waziwazi ulimwenguni. Mimi siku zote nimefundisha nyumbani mwa kuombea napo Patakatifu, Wayuda wote wanapokusanyika; hakuna, nililolisema na kufichaficha,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nalifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala kwa siri mimi sikusema neno lo lote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akamujibu: “Nilisema na watu wote waziwazi, nilifundisha siku zote katika nyumba za kuabudia na katika hekalu, pahali Wayuda wote wanapokutana. Sikusema kitu kwa uficho.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu kwa wazi; mimi siku zote nalifundisha katika masunagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi siku zote; wala kwa siri sikusema neno.