John 18:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro alikuwa hapo akiota moto. Basi, wakamwuliza, “Je, nawe pia si mmoja wa wanafunzi wake?” Yeye akakana na kusema, “Si mimi!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo Simoni Petro alikuwa amesimama akiota moto. Baadhi ya watu waliokuwepo wakamuuliza, “Je, wewe si mmoja wa wanafunzi wake?” Petro akakana, akasema, “Sio mimi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Simoni Petro alikuwa akisimama huko, anakota moto. Basi wakamwambia, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmojawapo? Naye akakana, akasema, Si mimi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Simoni Petro alikuwa amesimama karibu na moto, akijipasha joto. Watu wengine wakamwambia Petro, “Je, wewe si mmoja wa wafuasi wa mtu yule?” Petro alikataa hilo. Akasema, “Hapana, mimi siye.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro alikuwa hapo akiota moto. Basi, wakamwuliza, “Je, nawe pia si mmoja wa wanafunzi wake?” Yeye akakana na kusema, “Si mimi!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro alikuwa hapo akiota moto. Basi, wakamwuliza, “Je, nawe pia si mmoja wa wanafunzi wake?” Yeye akakana na kusema, “Si mimi!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo Simoni Petro alikuwa amesimama akiota moto. Baadhi ya wale waliokuwepo wakamwuliza, “Je, wewe si mmoja wa wanafunzi wake?” Petro akakana, akasema, “Mimi sio.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo Simoni Petro alikuwa amesimama akiota moto. Baadhi ya wale waliokuwepo wakamuuliza, “Je, wewe si mmoja wa wanafunzi wake?” Petro akakana, akasema, “Sio mimi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Simoni Petro alikuwa akisimama huko, anaota moto. Basi wakamwambia, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmojawapo? Naye akakana, akasema, Si mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro alikuwa hapo akiota moto. Basi, wakamwuliza, “Je, nawe pia si mmoja wa wanafunzi wake?” Yeye akakana na kusema, “Si mimi!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Simoni Petero alikuwa amesimama akiota moto. Walipomwuliza: Wewe nawe humo miongoni mwao wanafunzi wake? akakana akisema: Simo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Simoni Petro alikuwa akisimama huko, anakota moto. Basi wakamwambia, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmojawapo? Naye akakana, akasema, Si mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule Simoni Petro alikuwa angali pale akiota moto. Basi wakamwuliza: “Wewe vilevile si mumoja wa wanafunzi wa mutu huyu?” Petro akakana, akisema: “Hapana! Mimi si mwanafunzi wake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Simon alikuwa akisimama, anakola moto. Bassi wakamwambia, Wewe nawe je! huwi mmojawapo wa wanafunzi wake? Yeye akanena, Sio mimi.