John 18:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yuda alichukua kikosi cha askari na walinzi kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaja nao bustanini wakiwa na taa, mienge na silaha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Yuda akaja kwenye bustani akiongoza kikosi cha askari Warumi, na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Nao walikuwa wamechukua taa, mienge na silaha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa hiyo Yuda akaongoza kundi la askari hadi katika bustani hiyo pamoja na walinzi wengine kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Hawa walikuwa wamebeba mienge, taa, na silaha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Yuda alichukua kikosi cha askari na walinzi kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaja nao bustanini wakiwa na taa, mienge na silaha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yuda alichukua kikosi cha askari na walinzi kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaja nao bustanini wakiwa na taa, mienge na silaha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Yuda akaja bustanini, akiongoza kikosi cha maaskari wa Kirumi na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo, wakiwa wamechukua taa, mienge na silaha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Yuda akaja bustanini. Aliongoza kikosi cha askari wa Kirumi, na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Nao walikuwa wamechukua taa, mienge na silaha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yuda alichukua kikosi cha askari na walinzi kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaja nao bustanini wakiwa na taa, mienge na silaha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, Yuda alipokwisha kupata kikosi cha askari na watumishi wa watambikaji wakuu na wa Mafariseo, akaenda kulekule, wakishika taa na mienge na selaha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yuda akatwaa kundi la waaskari pamoja na walinzi waliotumwa na wakubwa wa makuhani na Wafarisayo. Akakuja nao kwenye bustani wakibeba taa, mienge na silaha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Yuda akiisha kupokea kikosi cha askari, na watumishi waliotoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaenda huko na makandili na taa za mkono na silaha.