John 18:37 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Pilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pilato akamuuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Isa akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa, na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni: ili niishuhudie kweli. Mtu yeyote aliye wa kweli husikia sauti yangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pilato akasema, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akamjibu, “Uko sahihi unaposema kuwa mimi ni mfalme. Nami nilizaliwa kwa ajili ya hili: kuwaeleza watu juu ya kweli. Ni kwa sababu hii nalikuja ulimwenguni. Kila mmoja aliye wa upande wa kweli hunisikiliza.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo Pilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Pilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pilato akamwuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni ili niishuhudie kweli. Mtu ye yote aliye wa kweli husikia sauti yangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pilato akamuuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Isa akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa, na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Mtu yeyote aliye wa kweli husikia sauti yangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Pilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pilato akamwuliza: Basi, wewe u mfalme gani? Yesu akajibu: Wewe unavyosema, ndivyo: mimi ni mfalme. Niliyozaliwa, tena niliyojia ulimwenguni, ndiyo hii: niishuhudie iliyo ya kweli! Kila aliye na kweli huisikia sauti yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Pilato akamwuliza: “Ni kusema wewe ni mufalme?” Yesu akamujibu: “Wewe umesema kwamba mimi ni mufalme. Mimi nimezaliwa na kuja katika dunia kusudi nishuhudie ukweli. Wote wanaokuwa upande wa ukweli, wananisikiliza mimi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme bassi? Yesu akajibu, Wewe wanena ya kwamba mimi ni mfalme. Mimi nalizaliwa kwa ajili ya haya na kwa ajili ya haya nalikuja ulimwenguni, illi niishuhudie kweli. Killa aliye wa kweli hunisikia sauti yangu.