John 18:40 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo wakapiga kelele: “La! Si huyu ila Baraba!” Naye Baraba alikuwa mnyanganyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wao wakapiga kelele, wakajibu, “Si huyu mtu, bali tufungulie Baraba!” Yule Baraba alikuwa mnyang’anyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang'anyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakajibu kwa kupiga kelele wakisema, “Hapana, siyo yeye! Mwache huru Baraba!” (Baraba alikuwa jambazi.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo wakapiga kelele: “La! Si huyu ila Baraba!” Naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo wakapiga kelele: “La! Si huyu ila Baraba!” Naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wao wakapiga kelele wakisema, “Si huyu mtu bali tufungulie Baraba!” Basi Baraba alikuwa mnyang'anyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wao wakapiga kelele wakisema, “Si huyu mtu, bali tufungulie Baraba!” Yule Baraba alikuwa mnyang’anyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang'anyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo wakapiga kelele: “La! Si huyu ila Baraba!” Naye Baraba alikuwa mnyanganyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipopiga makelele tena wakisema: Huyu hatumtaki, twamtaka Baraba; naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang’anyi. i.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu wakalalamika kwa nguvu: “Hatutaki mutu huyu! Tunataka utufungulie Baraba!” (Yule Baraba alikuwa munyanganyi.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wakapiga kelele marra ya pili, wote pia, wakinena, Si huyu, bali Barabba. Nae Barabba alikuwa mnyangʼanyi.