John 18:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao wakamjibu, “Yesu Mnazareti!” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.” Msaliti Yuda alikuwa amesimama hapo pamoja nao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wao wakamjibu, “Isa Al-Nasiri.” Isa akawajibu, “Mimi ndiye.” (Yuda, aliyemsaliti, alikuwa amesimama pamoja nao.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakamjibu, “Yesu kutoka Nazareti.” Akawaambia, “Mimi ni Yesu.” (Yuda yule aliyehusika kumsaliti Yesu alikuwa amesimama hapo pamoja nao.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti!” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.” Msaliti Yuda alikuwa amesimama hapo pamoja nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao wakamjibu, “Yesu Mnazareti!” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.” Msaliti Yuda alikuwa amesimama hapo pamoja nao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” Yesu akawajibu, “Mimi ndiye.” Yuda, yule aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wao wakamjibu, “Isa Al-Nasiri.” Isa akawajibu, “Mimi ndiye.” Yuda, yule aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao wakamjibu, “Yesu Mnazareti!” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.” Msaliti Yuda alikuwa amesimama hapo pamoja nao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipomjibu: Yesu wa Nasareti, akawaambia: Ni mimi. Lakini naye Yuda mwenye kumchongea alikuwa amesimama pamoja nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamujibu: “Yesu wa Nazareti.” Yesu akawaambia: “Ni mimi.” Na Yuda, yule aliyekuwa amemutoa, alikuwa akisimama pale pamoja nao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akawaambia, Mimi ndiye. Yuda nae aliyemsaiiti alikuwa akisimama pamoja nao.