John 19:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Pilato aliposikia maneno hayo akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo “Sakafu ya Mawe” (kwa Kiebrania, Gabatha).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pilato aliposikia maneno haya, akamtoa Isa nje tena. Akaketi kwenye kiti chake cha hukumu, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe (kwa Kiebrania ni Gabatha).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pilato aliposikia maneno hayo, akamtoa nje Yesu na kumweka mahali palipoitwa “Sakafu ya Mawe.” (Kwa Kiaramu jina lake ni Gabatha.) Pale Pilato akaketi katika kiti cha hakimu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Pilato aliposikia maneno hayo akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo: “Sakafu ya Mawe” (kwa Kiebrania, Gabatha).
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Pilato aliposikia maneno hayo akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo “Sakafu ya Mawe” (kwa Kiebrania, Gabatha).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pilato aliposikia maneno haya akamtoa Yesu nje tena akaketi katika kiti chake cha hukumu, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe, kwa Kiebrania paliitwa Gabatha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pilato aliposikia maneno haya akamtoa Isa nje tena akaketi katika kiti chake cha hukumu, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe (kwa Kiebrania paliitwa Gabatha).
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Pilato aliposikia maneno hayo akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo “Sakafu ya Mawe” (kwa Kiebrania, Gabatha).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pilato alipoyasikia maneno haya akampeleka Yesu nje, akaketi katika kiti cha uamuzi mahali panapoitwa Kiwanja cha Mawe, lakini Kiebureo: Gabata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pilato aliposikia maneno haya, akamupeleka Yesu inje; akaikaa katika kiti cha hukumu kwenye nafasi inayoitwa katika Kiebrania “Gabata,” maana yake “Sakafu ya Mawe.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Pilato, aliposikia maneno haya, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti, mahali paitwapo Sakafu ya mawe, na kwa Kiebrania Gabbatha.