John 19:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, Pilato akamtia Yesu mikononi mwao ili asulubiwe. Basi, wakamchukua Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Pilato akamkabidhi Isa kwao ili wamsulubishe. Kwa hiyo askari wakamchukua Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo Pilato akamkabidhi Yesu kwao ili auawe juu ya msalaba. Askari wakamchukua Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, hapo Pilato akamtia Yesu mikononi mwao ili asulubiwe. Basi, wakamchukua Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, Pilato akamtia Yesu mikononi mwao ili asulubiwe. Basi, wakamchukua Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Pilato akamkabidhi Yesu kwao ili wamsulibishe. Kwa hiyo maaskari wakamchukua Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Pilato akamkabidhi Isa kwao ili wamsulubishe. Kwa hiyo askari wakamchukua Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulubiwe; nao wakampokea Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, Pilato akamtia Yesu mikononi mwao ili asulubiwe. Basi, wakamchukua Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, hapo ndipo, alipomtoa, awambwe msalabani. Wakampeleka Yesu;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Pilato akamutoa Yesu kwao, kusudi atundikwe juu ya musalaba. Basi wakamukamata Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi ndipo akamtia mikononi mwao asulibishwe. Bassi wakampokea Yesu: