John 19:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo “Fuvu la Kichwa” (kwa Kiebrania Golgotha).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa, akiwa ameubeba msalaba wake, akatoka kuelekea mahali palipoitwa Fuvu la Kichwa (kwa Kiebrania ni Golgotha).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye Yesu akaubeba msalaba wake hadi mahali panapoitwa “Fuvu la Kichwa”. (Kwa Kiaramu mahali hapo paliitwa “Golgotha”.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo “Fuvu la Kichwa”, (kwa Kiebrania Golgotha).
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo “Fuvu la Kichwa” (kwa Kiebrania Golgotha).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akiwa ameubeba msalaba wake, akatoka kuelekea mahali palipoitwa, Fuvu la Kichwa (ambapo kwa Kiebrania ni Golgotha).
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa, akiwa ameubeba msalaba wake, akatoka kuelekea mahali palipoitwa Fuvu la Kichwa (kwa Kiebrania ni Golgotha).
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akatoka, huku akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo “Fuvu la Kichwa” (kwa Kiebrania Golgotha).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
naye akajichukulia mwenyewe msalaba wake alipotoka kwenda mahali panapoitwa Fuvu la Kichwa, jina lake Kiebureo: Golgota.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akaondoka katika muji akibeba musalaba wake mpaka kwenye nafasi inayoitwa katika Kiebrania “Golgota”, maana yake: “Kilima cha Mufupa wa Kichwa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akatoka, akijichukulia msalaba wake, hatta mahali paitwapo pa kichwa, na kwa Kiebrania Golgotha;