John 19:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Askari walipokwisha msulubisha Yesu, walizichukua nguo zake, wakazigawa mafungu manne, fungu moja kwa kila askari. Walichukua pia na kanzu yake; kanzu hiyo ilikuwa imefumwa kwa kipande kimoja tu, bila mshono.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Askari walipokwisha kumsulubisha Isa, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono, bali limefumwa tangu juu hadi chini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo baada ya askari kumpigilia Yesu kwa misumari msalabani, walizichukua nguo zake na kuzigawa katika mafungu manne. Kila askari alipata fungu moja. Pia wakalichukua vazi lake lililokuwa limefumwa kwa kipande kimoja tu cha kitambaa kutoka juu hadi chini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Askari walipokwisha msulubisha Yesu, walizichukua nguo zake, wakazigawa mafungu manne, fungu moja kwa kila askari. Walichukua pia na kanzu yake; kanzu hiyo ilikuwa imefumwa kwa kipande kimoja tu, bila mshono.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Askari walipokwisha msulubisha Yesu, walizichukua nguo zake, wakazigawa mafungu manne, fungu moja kwa kila askari. Walichukua pia na kanzu yake; kanzu hiyo ilikuwa imefumwa kwa kipande kimoja tu, bila mshono.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Askari walipokwisha kumsulibisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Askari walipokwisha kumsulubisha Isa, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao askari walipomsulubisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Askari walipokwisha msulubisha Yesu, walizichukua nguo zake, wakazigawa mafungu manne, fungu moja kwa kila askari. Walichukua pia na kanzu yake; kanzu hiyo ilikuwa imefumwa kwa kipande kimoja tu, bila mshono.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Askari walipokwisha kumwamba Yesu msalabani wakayachukua mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kila askari fungu moja, wakaichukua hata kanzu. Lakini ile kanzu ilikuwa pasipo mshono, toka juu yote ilikuwa imefumwa tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waaskari walipokwisha kumutundika Yesu juu ya musalaba wakakamata nguo zake na kuzigawanya katika sehemu ine, wakimupa kila askari sehemu moja. Wakakamata vilevile kanzu yake iliyokuwa bila mushono, iliyofumwa kwa kipande kimoja tu tokea juu mpaka chini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi askari, walipomsulibisha Yesu, wakatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu mane, kwa killa askari fungu lake; nayo kanzu: na kanzu ile haikushonwa, imefumwa pia tangu juu.