John 19:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, hao askari wakashauriana: “Tusiipasue, ila tuipigie kura itakuwa ya nani.” Jambo hilo lilifanyika ili yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: “Waligawana mavazi yangu, na nguo yangu wakaipigia kura.” Basi, ndivyo walivyofanya hao askari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaambiana, “Tusilichane ila tulipigie kura ili kuamua ni nani atalichukua.” Hili lilitukia ili Maandiko yapate kutimizwa yale yaliyosema, “Wanagawana nguo zangu, na vazi langu wanalipigia kura.” Hayo ndiyo waliyoyafanya wale askari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo askari wakasemezana wao kwa wao, “Hatutalichana vazi hili vipande vipande. Hebu tulipigie kura kuona nani atakayelipata.” Hili lilitokea ili kuweka wazi maana kamili ya yale yanayosemwa katika Maandiko: “Waligawana miongoni mwao mavazi yangu, na wakakipigia kura kile nilichokuwa nimevaa.” Hivyo ndivyo maaskari walivyofanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, hao askari wakashauriana: “Tusiipasue, ila tuipigie kura itakuwa ya nani.” Jambo hilo lilifanyika ili yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: “Waligawana mavazi yangu, na nguo yangu wakaipigia kura.” Basi, ndivyo walivyofanya hao askari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, hao askari wakashauriana: “Tusiipasue, ila tuipigie kura itakuwa ya nani.” Jambo hilo lilifanyika ili yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: “Waligawana mavazi yangu, na nguo yangu wakaipigia kura.” Basi, ndivyo walivyofanya hao askari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaambiana, “Tusilichane ila tulipigie kura ili kuamua ni nani alichukue.” Hili lilitukia ili Maandiko yapate kutimizwa yale yaliyosema, “Waligawana nguo zangu na mavazi yangu wakayapigia kura.” Hayo ndiyo waliyoyafanya wale askari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaambiana, “Tusilichane ila tulipigie kura ili kuamua ni nani atalichukua.” Hili lilitukia ili Maandiko yapate kutimizwa yale yaliyosema, “Wanagawana nguo zangu, na vazi langu wanalipigia kura.” Hayo ndiyo waliyoyafanya wale askari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, hao askari wakashauriana: “Tusiipasue, ila tuipigie kura itakuwa ya nani.” Jambo hilo lilifanyika ili yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: “Waligawana mavazi yangu, na nguo yangu wakaipigia kura.” Basi, ndivyo walivyofanya hao askari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo wakaambiana: Tusiipasue, ila tuipigie kura, ajulike atakayeipata. Imekuwa hivyo, litimie lililoandikwa: Wakajigawanyia nguo zangu, nalo vazi langu zuri wakalipigia kura. Ndio askari waliofanya hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waaskari wakaambiana: “Tusipasue kanzu hii, lakini tuipigie kura, kusudi tujue itakuwa ya nani.” Mambo haya yalifanyika kusudi Maandiko Matakatifu yanayosema hivi yatimie: “Waligawanya nguo zangu nayo kanzu yangu wakaipigia kura.” Mambo hayo ndiyo waaskari waliyofanya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani; andiko litimie linenalo, Waligawanya nguo zangu, na vazi langu walilipigia kura. Bassi ndivyo walivyofanya askari.