John 19:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Karibu na msalaba wa Isa walikuwa wamesimama mama yake, na dada wa mamaye, na Mariamu mke wa Klopa, na Mariamu Magdalene.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mama yake Yesu alisimama karibu na msalaba wa mwanawe, Dada yake mamaye Yesu pia alikuwa amesimama pale pamoja na Mariamu mke wake Kleopa, na Mariamu Magdalena.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo huo karibu na msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama: Maria mama yake, Maria dada wa mamaye, yaani, mke wa Klopa na Maria Magdalene.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo huo karibu na msalaba wa Isa walikuwa wamesimama mama yake, na dada wa mamaye, na Maria mke wa Klopa, na Maria Magdalene.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini penye msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama akina mama yake na ndugu ya mama yake, jina lake Maria wa Klofa, na Maria Magadalene.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mama ya Yesu, dada ya mama yake, Maria muke wa Kleopa na Maria wa muji wa Magdala walikuwa wamesimama karibu na musalaba wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na penye msalaba wake Yesu wamesimama mama yake, na ndugu ya mama yake, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.