John 19:28 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Yesu aliona kwamba yote yalikuwa yametimia; na, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia, akasema, “Naona kiu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya haya, akijua kuwa mambo yote yamemalizika, na ili kutimiza Maandiko, Isa akasema, “Naona kiu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadaye, Yesu akajua kuwa kila kitu kimekwisha kamilika. Ili kuyafanya Maandiko yatimie akasema, “Nina kiu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alijua kwamba yote yalikuwa yametimia; na, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia, akasema, “Naona kiu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Yesu aliona kwamba yote yalikuwa yametimia; na, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia, akasema, “Naona kiu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya haya, Yesu hali akijua kuwa mambo yote yamemalizika, alisema ili kutimiza Maandiko, “Naona kiu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya haya, Isa hali akijua kuwa mambo yote yamemalizika, alisema ili kutimiza Maandiko, “Naona kiu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Yesu aliona kwamba yote yalikuwa yametimia; na, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia, akasema, “Naona kiu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baadaye Yesu alipojua, ya kuwa yote yamekwisha timizwa, akasema: Nina kiu, kwamba nayo hayo yaliyoandikwa yapate kutimia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Yesu akiwa anajua kwamba mambo yote yametimia, akasema hivi kusudi Maandiko Matakatifu yatimie: “Ninasikia kiu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baada ya haya Yesu, akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizwa, andiko litimizwe, akasema, Nina kiu.