John 19:39 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Nikodemo ambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu usiku, akaja akiwa amechukua mchanganyiko wa manemane na ubani kiasi cha kilo thelathini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Nikodemo, yule ambaye kwanza alimwendea Isa usiku, akaja, akaleta mchanganyiko wa manemane na manukato, yenye uzito wa zaidi ya kilo thelathini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaenda Nikodemo naye, (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza), akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratli mia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nikodemu akaenda pamoja na Yusufu. Nikodemu, alikuwa ni yule mtu aliyekuja kwa Yesu hapo kabla na kuzungumza naye usiku. Huyu alileta kadiri ya lita mia moja ya marashi yenye mchanganyiko wa manemane na uvumba.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye Nikodemo ambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu usiku, akaja akiwa amechukua mchanganyiko wa manemane na ubani kiasi cha kilo thelathini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Nikodemo ambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu usiku, akaja akiwa amechukua mchanganyiko wa manemane na ubani kiasi cha kilo thelathini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Nikodemo, yule ambaye kwanza alimwendea Yesu usiku, akaja, akaleta mchanganyiko wa manemane na manukato, yenye uzito wa zaidi ya kilo thelathini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Nikodemo, yule ambaye kwanza alimwendea Isa usiku, akaja, akaleta mchanganyiko wa manemane na manukato, yenye uzito wa zaidi ya kilo thelathini
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaenda Nikodemo naye, (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza), akaleta mchanganyiko wa manemane na uudi, yapata ratili mia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Nikodemo ambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu usiku, akaja akiwa amechukua mchanganyiko wa manemane na ubani kiasi cha kilo thelathini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pakaja Nikodemo naye, ni yule aliyemjia usiku hapo kwanza, akaleta manemane iliyochanganyika na uvumba, yapata kama mizigo miwili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaenda Nikodemo naye, (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza), akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratli mia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Nikodemo, yule aliyemwendea Yesu siku moja usiku, alikuja vilevile. Alikuwa akileta yapata kilo makumi tatu ya marasi yaliyochangwa na udi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaenda Nikodemo nae, yule aliyemwendea usiku hapo kwanza, akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratli mia.