John 19:40 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, waliutwaa mwili wa Yesu, wakaufunga sanda pamoja na manukato kufuatana na desturi ya Wayahudi katika kuzika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakauchukua mwili wa Isa, wakaufunga katika sanda ya kitani safi pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu hawa wawili wakauchukua mwili wa Yesu na wakauzungushia vipande vya sanda ya kitani pamoja na marashi yale. (Hivi ndivyo Wayahudi walivyowazika watu.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, waliutwaa mwili wa Yesu, wakaufunga sanda pamoja na manukato kufuatana na desturi ya Wayahudi katika kuzika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, waliutwaa mwili wa Yesu, wakaufunga sanda pamoja na manukato kufuatana na desturi ya Wayahudi katika kuzika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakauchukua mwili wa Yesu, wakauviringishia sanda ya kitani safi pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakauchukua mwili wa Isa, wakaufunga katika sanda ya kitani safi pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, waliutwaa mwili wa Yesu, wakaufunga sanda pamoja na manukato kufuatana na desturi ya Wayahudi katika kuzika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakautwaa mwili wa Yesu, wakaufunga kwa sanda pamoja na yale manukato, kama Wayuda walivyozoea kuzika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wote wawili wakatwaa maiti ya Yesu, wakaifunga na vitambaa vyenye kupakaliwa mafuta zenye harufu nzuri sawa na desturi za maziko za Wayuda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wakautwaa mwili wa Yesu, wakaufunga saanda ya bafta, pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika.