John 19:41 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mahali hapo aliposulubiwa Yesu palikuwa na bustani, na katika bustani hiyo kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakutiwa bado mtu yeyote ndani yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi palikuwa na bustani karibu na mahali pale aliposulubiwa, na pale ndani ya ile bustani palikuwa na kaburi jipya, ambalo halikuwa limezikiwa mtu bado.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na pale pale aliposulibiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani mna kaburi jipya, ambalo hajatiwa bado mtu ye yote ndani yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pale msalabani sehemu alipouawa Yesu, palikuwepo na bustani. Katika bustani ile palikuwemo na kaburi jipya la kuzikia. Hakuna mtu aliyewahi kuzikwa ndani ya kaburi lile.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mahali hapo aliposulubiwa Yesu palikuwa na bustani, na katika bustani hiyo kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakutiwa bado mtu yeyote ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mahali hapo aliposulubiwa Yesu palikuwa na bustani, na katika bustani hiyo kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakutiwa bado mtu yeyote ndani yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi palikuwa na bustani karibu na mahali pale aliposulibiwa, nako ndani ya ile bustani palikuwa na kaburi jipya, ambalo hajazikiwa mtu bado.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi palikuwa na bustani karibu na mahali pale aliposulubiwa, na pale ndani ya ile bustani palikuwa na kaburi jipya, ambalo halikuwa limezikiwa mtu bado.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na pale pale aliposulubiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani mna kaburi jipya, ambalo hajatiwa bado mtu yeyote ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mahali hapo aliposulubiwa Yesu palikuwa na bustani, na katika bustani hiyo kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakutiwa bado mtu yeyote ndani yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mahali pale, alipowambwa msalabani palikuwa na kiunga, namo mle kiungani mlikuwa na kaburi jipya, ambalo hajazikwa mtu bado ndani yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na pale pale aliposulibiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani mna kaburi jipya, ambalo hajatiwa bado mtu ye yote ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa bustani pale walipomutundika Yesu, na katika bustani ile kulikuwa kaburi jipya, mulimokuwa hamujazikwa mutu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mahali pale aliposulibiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani kaburi jipya, bado hajatiwa mtu aliye yote ndani yake.