John 2:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huu ndio muujiza wa kwanza wa Isa; aliufanya huko Kana ya Galilaya. Hivyo Isa alidhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ishara hii ilikuwa ya kwanza aliyoifanya Yesu katika mji wa Kana ya Galilaya. Kwa hili Yesu alionesha ukuu wake wa kimungu, na wafuasi wake wakamwamini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonyesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huu, ndio uliokuwa mwujiza wa kwanza Yesu aliofanya huko Kana ya Galilaya. Hivyo Yesu alidhihirisha utukufu wake na wanafunzi wake wakamwamini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huu, ndio uliokuwa muujiza wa kwanza Isa aliofanya Kana ya Galilaya. Hivyo Isa alidhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huo ndio mwanzo wa vielekezo, Yesu alivyovifanya, nao ulifanyika Kana wa Galilea; ndivyo, alivyoufunua utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamtegemea.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni vile Yesu alivyofanya kitambulisho chake cha kwanza katika Kana ya Galilaya. Pale alionyesha utukufu wake na wanafunzi wake wakamwamini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwanzo huu wa ishara Yesu alifanya Kana ya Galilaya, akauonyesha utukufu wake, wanafunzi wake wakamwamini.