John 2:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akawakuta mle hekaluni watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huko uani la Hekalu aliwakuta watu wakiuza ng’ombe, kondoo na njiwa, nao wengine walikuwa wameketi mezani wakibadili fedha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika eneo la Hekalu aliwaona watu wakiuza ng'ombe, mbuzi na njiwa. Aliwaona wengine wakikalia meza na kufanya biashara ya kubadili fedha za watu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akawakuta mle hekaluni watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huko Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa na wengine walikuwa wameketi mezani wakibadili fedha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huko Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng’ombe, kondoo na njiwa, nao wengine walikuwa wameketi mezani wakibadili fedha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akawakuta mle hekaluni watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoona hapo Patakatifu wenye kuuzia palepale ng'ombe na kondoo na njiwa, hata wavunjaji wa fedha waliokuwapo wamekaa,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akakuta watu katika hekalu wakiuzisha ngombe, kondoo na njiwa, na wengine wenye kubadilisha feza wakiikaa kwenye meza zao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaona hekaluni watu waliokuwa wakiuza ngʼombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi;