John 2:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadhi ya Wayahudi wakamwuliza Yesu, “Utafanya mwujiza gani kuonesha kwamba unayo haki kufanya mambo haya?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Wayahudi wakamuuliza, “Unaweza kutuonesha ishara gani ili kuthibitisha mamlaka uliyo nayo ya kufanya mambo haya yote?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya Wayahudi wakamwambia Yesu, “Tuoneshe muujiza mmoja kama ishara kutoka kwa Mungu. Thibitisha kwamba unayo haki ya kufanya mambo haya.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baadhi ya Wayahudi wakamwuliza Yesu, “Utafanya muujiza gani kuonyesha kwamba unayo haki kufanya mambo haya?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadhi ya Wayahudi wakamwuliza Yesu, “Utafanya mwujiza gani kuonesha kwamba unayo haki kufanya mambo haya?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Wayahudi wakamwuliza, “Unaweza kutuonyesha ishara gani ili kuthibitisha mamlaka uliyo nayo ya kufanya mambo haya?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Wayahudi wakamuuliza, “Unaweza kutuonyesha ishara gani ili kuthibitisha mamlaka uliyo nayo ya kufanya mambo haya?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuoneshayo, kwamba unafanya haya?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadhi ya Wayahudi wakamwuliza Yesu, “Utafanya mwujiza gani kuonesha kwamba unayo haki kufanya mambo haya?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa ajili ya Nyumba yako wivu unanila!* Wayuda walipomwuliza wakimwambia: Unatuonyesha kielekezo gani, kwa kuwa unafanya hivyo?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Wayuda wakamwuliza: “Utaonyesha kitambulisho gani kwa kutuhakikishia kwamba uko na haki ya kufanya hivi?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Wayahudi wakajibu wakamwambia, Ishara gani utuonyeshayo, iwapo unafanya haya?