John 2:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, alipofufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake walikumbuka kwamba alikuwa amesema hayo, wakayaamini Maandiko Matakatifu na yale maneno ambayo Yesu alikuwa amesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kufufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka yale aliyokuwa amesema. Ndipo wakayaamini Maandiko na yale maneno Isa alikuwa ameyasema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya kufufuliwa kutoka katika wafu, wafuasi wake wakakumbuka kwamba alikuwa ameyasema hayo. Hivyo wakayaamini Maandiko, na pia wakayaamini yale aliyoyasema Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, alipofufuliwa kutoka wafu, wanafunzi wake walikumbuka kwamba alikuwa amesema hayo, wakaamini Maandiko Matakatifu na yale maneno aliyokuwa akisema Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, alipofufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake walikumbuka kwamba alikuwa amesema hayo, wakayaamini Maandiko Matakatifu na yale maneno ambayo Yesu alikuwa amesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kufufuka kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka yale aliyokuwa amesema. Ndipo wakayaamini Maandiko na yale maneno Yesu aliyokuwa amesema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kufufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka yale aliyokuwa amesema. Ndipo wakayaamini Maandiko na yale maneno Isa aliyokuwa amesema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, alipofufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake walikumbuka kwamba alikuwa amesema hayo, wakayaamini Maandiko Matakatifu na yale maneno ambayo Yesu alikuwa amesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, alipokwisha kufufuliwa katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka, ya kuwa aliyasema hayo. Wakayategemea Maandiko na neno hilo, Yesu alilolisema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Yesu alipokwisha kufufuka, wanafunzi wake wakakumbuka kwamba alikuwa anasema juu ya jambo lile, wakaamini Maandiko Matakatifu na maneno yale aliyosema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi alipofufuliwa katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa amenena neno hili, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.