John 2:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi hapo palikuwa na mitungi sita iliyotengenezwa kwa mawe; iliwekwa hapo kwa ajili ya desturi ya Kiyahudi ya kujitakasa; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mahali hapo ilikuwepo mitungi mikubwa sita iliyotengenezwa kwa mawe iliyotumiwa na Wayahudi katika desturi yao maalumu ya kunawa. Kila mtungi mmoja ulikuwa na ujazo wa lita 80 au 120.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi ilikuwapo huko mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi, kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi ilikuwepo mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kunawa, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pale palikuwa na mitungi sita ya mawe iliyokuwa imewekwa kwa desturi ya kunawa kwao Wayuda; kila mmoja ulienea mabuyu mawili au matatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pale kulikuwa mitungi sita iliyotengenezwa kwa mawe iliyotumiwa na Wayuda kwa kutilia maji ya kujitakasa. Ndani ya kila mumoja kuliweza kuingia yapata litre mia moja za maji.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Palikuwako mabalasi sita ya mawe, yamewekwa huko kwa desturi ya kutawaza kwao Wayahudi, killa moja lapata kadiri ya nzio mbili au tatu.