John 2:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akawaambia, “Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kidogo; mpelekeeni mkuu wa sherehe.” Hivyo wakachota, wakampelekea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kiasi na mumpelekee mkuu wa sherehe.” Nao wakafanya kama walivyoambiwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akawaambia, “Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akawaambia, “Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza.” Hivyo wakachota, wakampelekea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza.” Hivyo wakachota, wakampelekea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa sherehe. Wakapeleka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akawaambia, “Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akawaambia: Sasa tekeni, mmpelekee mwandaliaji! Basi, wakampelekea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yesu akamwambia: “Muteke sasa kwa maji haya na muyapeleke kwa mukubwa wa karamu.” Watumishi wakayapeleka
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia, Sasa tekeni, mpelekeeni mkuu wa meza. Wakapeleka.