John 20:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, kulipokuwa bado giza, Mariamu Magdalene alienda kaburini na kukuta lile jiwe limeondolewa penye ingilio.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Asubuhi na mapema siku ya Jumapili, wakati bado lilikuwepo giza, Mariamu Magdalena akaenda kwenye kaburi la Yesu. Naye akaona kuwa lile jiwe kubwa lilikuwa limeondolewa kutoka mlangoni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, kulipokuwa kungali giza bado, Maria Magdalene alikwenda kaburini na kukuta lile jiwe limeondolewa penye ingilio.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, kulipokuwa kungali giza bado, Maria Magdalene alikwenda kaburini na kukuta lile jiwe limeondolewa penye ingilio.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kukiwa bado giza; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya kwanza ya juma Maria Magadalene akaenda mapema kaburini, kukingali gizagiza. Alipoliona lile jiwe, limekwisha ondolewa kaburini,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya kwanza ya juma asubui mapema, kulipokuwa kungali giza, Maria wa Magdala akaenda kwenye kaburi. Alipofika kule akaona kama jiwe lililofunika kaburi limeondolewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
HATTA siku ya kwanza ya sabato Mariamu Magdalene akaenda kaburini alfajiri, kungali giza bado, akaliona jiwe limeondolewa kaburini.